Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

HALI BADO TETE NCHINI UFARANSA



 

Mechi ya kirafiki kati ya Ubelgiji na Uhispania ambayo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa leo mjini Brussels Ubelgiji imeahirishwa kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea jijini Paris Ufaransa Ijumaa iliyopita.

Takriban watu 129 walipoteza maisha yao baada ya wavamizi wa kujitolea muhanga kujaribu kuingia katika uwanja wa Stade de France ambapo Ugerumani ilikuwa mgeni wa Ufaransa miongoni mwa maeneo mengi 5 jijini humo.

Mechi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa katika uwanja wa King Baudouin .
Maafisa wanaongoza shughuli za upelelezi tayari wamemtaja raia moja wa Ubelgiji kuwa ndiye aliyepanga njama hiyo ya uvamizi huku vyombo vya usalama vikimtaja mzaliwa wa Ubelgiji Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26, kuwa mshukiwa mkuu wa miripuko hiyo.

Serikali ya Ubelgiji tayari imeimarisha ulinzi ikihofia kutokea kwa shambulizi kama lile la Paris.

Shirikisho la kandanda la Ubelgiji limesema kuwa limechukua tahadhari hiyo kabla ya athari kufuatia mauaji ya zaidi ya watu 129.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget