
MSHAMBULIAJI nyota wa Leicester City, Jamie Vardy
ambaye ndio mfungaji anayeongoza kwasasa katika Ligi Kuu, ametajwa kuwa
mchezaji bora wa mwezi Octoba baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa
miaka 28, ameafunga mabao 12 katika mechi 12 za ligi msimu huu huku akifunga
katika mechi tisa zilizopita na kuisaidia Leicester kukaa katika nafasi ya
tatu.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger yeye ameteuliwa
kuwa meneja bora wa mwezi baada ya kushinda mechi nne alizosimamia mwezi
uliopita na kukifanya kikosi chake kukaa katika nafasi ya pili katika msimamo
wa ligi.
Hiyo inakuwa tuzo ya 15 kwa Wenger toka aanze kuinoa
Arsenal.
Wenger mwenye umri wa miaka 66, alimshinda meneja wa Leicester Claudio
Ranieri ambaye yeye ameshinda mechi mechi tatu mwezi uliopita.
Post a Comment