Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

STARS KUREJEAN LEO NYUMBANI.



 
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatajia kurejea leo nyumbani na itafikia katika Hotel ya Serena jinni Dar es Salaam ambapo itaweka kambi kwaajili ya mchezo wake wa jumamosi dhidi ya Algeria.


Stars iliyokuwa imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa takribani siku 10, inarejea nyumbani ikiwa imefanya mazoezi vizuri kujiandaa na kuwakabili Mbweha wa Jangwani Algeria siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongelea kuhusu kambi kocha wa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukru kwa kambi waliyoipata Afrika Kusini, wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi katika kiwango cha juu, hapakua na majeruhi hivyo ana imani vijana wake watafanya vizuri siku ya Jumamosi.

Mkwasa amewaomba watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwasapoti katika mchezo dhidi ya Algeria, uwepo wa watanzania wengi uwanjani kuwashangilia utaongeza morali zaidi kwa wachezaji watakaokuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania.

Mara baada ya kuwasili leo kikosi cha Mkwasa kitafanya mazoezi kesho Alhamis jioni katika uwanja wa Taifa, na Ijumaa yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabisa ya mchezo wenyewe unaosubiriwa kwa hamu.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget