Ndege iliyobeba abiria imeanguka karibu na mji wa
Medellin nchini Colombia ikiwa imebeba abiria 72 kati yao wakiwa ni wachezaji
wa timu ya daraja la kwanza nchini Brazil ya Sudamericana.
Imeelezwa kwamba watu nane tu wameokoka na bado
haijajulikana ni akina nani kwa kuwa ndege hiyo imeanguka katika sehemu mbaya
ambayo ilinyesha mvua kubwa.
Meya wa jiji la Medellin, Federico Gutierrez
amethibitisha kudondoka kwa ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria hao 72 pamoja
na wafanyakazi wanane.
Kikosi cha Sudamericana kutoka Kusini mwa Brazil
kilikuwa katika ndege hiyo ya Lamia yenye makao yake makuu nchini Bolivia
kwenda Medellin kucheza mechi ya dhidi Atletico Nacional.
Post a Comment