Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

Makoma: kundi la muziki wa injili lililoteka nyoyo za watu miaka ya 90.



Image result for historia ya kundi la makoma

Na Nicolaus Kilowoko

Tunapotaja waimbaji wa nyimbo za injili ambao wamewahi kutamba katika tasnia ya Sanaa ya muziki ulimwenguni huwezi kuacha kulitaja kundi la Makoma. 

Makoma ni kundi la muziki wa injili ambalo lilihusisha nyimbo za muziki wa maadhi ya rumba,pop na R&B ambalo lilianzishwa mjini Kinshasa, katika nchi ya kidemokrasia ya Congo na kuweza kukua zaidi nchini Uholanzi.

Kundi hili lilikuwa linahusisha ndugu sita wakiwemo wakaka watatu na wadada watutu akiwemo Nathalie Makoma, Annie Makoma, Pengani Makoma, Tutala Makoma, Duma Makoma, Martin Makoma pamoja na rafiki yao mwingine alikuwa anajulikana kama Patrick Badine.

Kundi hili liliweza kuitikisa sana dunia kipindi hicho cha miaka ya 2000 kwa nyimbo zao hasa kwa wapenzi wa muziki wa injili na hata wale wanaosikiliza nyimbo za kidunia. 

Kundi hili pia liweza kukua zaidi baada ya kuanzishwa na Tutala Makoma mnamo mwaka 1993, na kuweza kutumbuiza majukwaani kama kundi mwaka 1995 na wakati huo likijulikana kwa jina la "Nouveau Testament".

Na siku zote waliweza kutumia Lugha ya kilingala pamoja na kiingereza lakini pia waliweza kutumia kifaransa,kiholanzi na Kijerumani kwa wakati mwingine.

Familia hii ilifanikiwa kuondoka nchini Congo zamani ikijulikana kama Zaire kutokana na matatizo ya kisiasa na waliweza kuelekea nchini Uholanzi ambapo baadae walielekea nchini Ujerumani lakini baadae waliweza kurudi nchini Uholanzi mwaka 1996.

Wakati huo wakijulikana kama “Nouveau Testament”The walifanikiwa kubadirisha jina hilo na kuamua kutumia jina la familia lilojulikana kama Makoma na kuweza kukua zaidi barani Ulaya.

Makoma waliweza kufanikiwa kurekodi katika studio ambazo zilikuwa zikimilikiwa na ndugu yao Tutala Makoma huku kazi ya kuwaremba ndugu hao ikifanywa na Annie Makoma na Martin Makoma aliweza kutengeneza mazingira mazuri ya picha na jukwaani.

Na albamu yao ya kwanza kuitoa ilikuwa ni mwaka 2000 iliyojulikana kama “Nzambe Na Bomoyi” (jesus for life), albam hii ndiyo iliyowapa umaarufu na kukamata tasnia ya muziki wa injili ikitamba kwa nyimbo kama Napesi, Butu na moyi, Mwinda, Moto oyo, Natamboli ikifuatiwa na albamu nyingine ya “On Faith” mwaka 2002. 

Mwaka huo wa 2002 Makoma walifanikiwa kushinda tuzo ya kundi bora kutoka barani Afrika zilizokuwa zikisimamiwa na “Kora African Music Awards” na kuweza kuwafanya kuzunguka nchi nyingi za barani Ulaya,Afrika na Canada.

Kundi la Makoma limeweza kusaini katika lebo ya muziki ya “Media Limited, international record” huku Makao Makuu yake yakiwa ni nchini Uingereza na Philipp Bauss akiwa ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo akiwa anazalisha kazi zote za video na nyimbo katika studio zake mwenyewe.

Harakati za kundi hilo hazikuishia hapo kwani mwaka huo huo wa 2002 walitoa albamu yao nyingine ya “Mokonzi na Bakonzi” ikiwa na maana mfalme wa wafalme ikibeba nyimbo zilizoimbwa kwa kilingala kama vile Nasengi,Bana, Naleli,Nzambe na Ngai na Tolingana. 

Mwaka 2005 walifyatuan albamu nyingine ya “Nzambe te” ikiwa na nyimbo kama Bomoyi te wakichanganya Kilingala na kiingereza huku kundi hili lilitamba na kuwafanya kuendelea kuwa juu katika muziki huko nchini uholanzi wakiimba bila ndugu yao Nathalie.

Kuvunjika kwa kundi la Makoma.

Kiongozi wa kundi hili alikuwa ni Nathalie Makoma ambaye aliliacha kundi hili mnamo mwaka 2004 na kuanza kuimba mwenyewe muziki wa kidunia na kufanya kazi za kuimba akiwa peke yake na kuweza kutengeneza matamasha mwaka 2006.

Nathalie Makoma, alizaliwa mnamo mwaka 1982 mjini Kinshasa na kufanikiwa kuwa mwimbaji mzuri sana nchini Uholanzi na kuweza kufanikiwa kuachia nyimbo ka “On Faith”mwaka 2003 na “I Saw the Light” mwaka 2005.

Nathalie alianza kuimba mwaka 1993 katika bendi yao ilijulikana kama "Nouveau Testament" kabla kujiunga na makoma alipofikisha miaka 14 alihamia uholanzi na kupata elimu ya kulitawala jukwaa katika chuo cha rockacademie huko Tilburg. 

Baada ya kundi la Makoma kuzunguka duniani na kupata mafanikio nathalie aliacha shule rasmi na kuzunguka na kundi hilo akitangaza injili kwa njia ya uimbaji. 

Nathalie baada ya kulikacha kundi hilo na kuamua kuimba muziki wa kidunia akiwa nje ya kanisa kutokana na kile alichodai kutaka kufanya kazi nyingine, huku wajuzi wa mambo wakidaiwa kuwa ni ugomvi baina yake na kaka yake mkubwa.

Mwaka 2007-2008, aliweza kurudi nchini Uholanzi na kuweza kufanya kazi zake kule kabla ya baadae kuweza kusaini mkataba na lebo ya Sony BMG.

Kurudi kwa Kundi la Makoma bila Nathaelie.

Kundi hili la Makoma liliweza kurudi tena na kutengeneza albam yao mpya mnamo mwaka 2012 ambayo ilijulikana kama Evolution ikihusisha nyimbo takribani 10.

Albamu ya Evolution waliyoitoa ilikuwa na nyimbo kumi, kama vile Evolution, Alingi biso, Yo ozali, Ndeko, Mokonzi, Se ye, Maboko Likolo, Mokili, Sosola na Nguya. 

Albamu hiyo ambayo ni ya kwanza tangu waungane imeweza kufanya vizuri kwenye vituo vya radio nchini kwao walikozaliwa pamoja na nchini nyingine duniani bila kusahau Afrika ya Mashariki na kati.

Na albamu yao ya tano ya My sweet lord waliyofanya kama kundi waliweza kumshirikisha Nathalie kama mwimbaji anayejitegemea.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget