Halloween Costume ideas 2015

KILOWOKO

Latest Post

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.



Image result for neymar 
Msimu wa majira ya joto hauwezi kupita bila ya James Rodriguez, Gareth Bale na Neymar kujaribu kuondoka katika klabu kubwa mbili za Hispania kutua Manchester United kucheza na Phil Jones.

Mapema juma hili, habari zimesambaa kuwa uhamisho wa Rodriguez kwenda Old Trafford utathibitika Jumapili na kwamba Gareth Bale, kupitia wawakilishi wake ameweka bayana kuwa anataka kuwa sehemu ya kikosi cha Jose Mourinho ikiwa ataondoka Real Madrid.

Sasa, kwa mujibu wa habari nyingine, Neymar naye anaweza kuwa kwenye mchakato wa kutua Manchester United pia.

Ripoti zinadai kuwa United wanataka kumleta nyota huyo Old Trafford kwani Jose Mourinho ataendelea kutumia fedha zaidi kuisuka Man United mpya na kuirejeshea hadhi yake Ulaya.



Image result for diamond platnumz akiimba 
Na Nicolaus Kilowoko

Muimbaji siku zote ni mburudishaji wa nafsi za watu na kuwafanya watu waburudike kwa kusikiliza muziki mzuri ambao unaambatana na vionjo mbalimbali vya muziki ikiwemo viombo vya muziki huo lakini pia hata sauti ya Muimbaji huyo.

Muimbaji unaweza kuimba kutokana na kuirushusu misuli yako vyema lakini pia kutoa sauti iliyo bora zaidi kutoka kinywani na kufanya sauti yako kuwa na mvuto wa aina yake.

Waimbaji wengi wamekuwa wakitengeneza sauti zao kwa kuimba sehemu zilizo wazi,kukimbia,lakini wengine wakifanya mazoezi ya kupiga push up,huku wengine wakila vyakula ambavyo vimekuwa haviwasaidii sana.

Siku zote tumekuwa tukiwafahamu waimbaji mbalimbali lakini leo hebu tujaribu kuona ni jinsi gani muimbaji anaweza kuwa na sauti nzuri na kuweza kuendelea kuwaburudisha mashabiki wake kwa kuzingatia vyakula vifauatavyo.

Kwa kujali miili ya waimbaji lazima utambue mwili wako lazima ujengwe kwa chakula bora na kuna vyakula ambayo muimbaji unapaswa kuvizingatia kuhakikisha hauvitumii na kuna vyakula ambavyo unapaswa uvitumie ili kuweza kuilinda sauti yako kuwa nzuri na kuendelea kuwaburudisha mashabiki wao.

Vyakula ambayo muimbaji unapswa kula kabla ya kutumbuiza.

Kuna vyakula ambavyo unaweza ukavifurahia kula kabla ya kufanya onyesho lako na kuifanya sauti yako iwe nzuri na yenye mvuto zaidi lakini pia haipaswi ule kupita kiasi.

Siku zote muimbaji unapaswa kuangalia na kuweka uwiano wa vyakula hivi wakati wa kula kwa kuzingati kuimarisha mwili lakini kuifanya sauti yako pia kuwa nzuri na hata nguvu mwilini.

Kuna vyakula ambayo unatakiwa uvitumie kwa wakati wote kwa kuimarisha sauti yako kwa kuchagua matunda ambayo ni mazuri kuliko kunywa juisi kutokana na kuwa yanaenda moja kwa moja katika mfumo wako wa damu na kufanya damu kutembea kwa haraka na kuifanya sauti yako itoke yenye uharisia.

Chakula kama nyama ya kuku kwanza inaongeza protini nyingi mwilini na kumfanya muimbaji kupata nguvu ambayo inayokufanya utoe sauti iliyokuwa na nguvu ya kutosha pasipo kubanwa.

Nyama ya samaki kama ambavyo ilivyo kwa nyama ya kuku pia inaongeza protini mwilini, kwa kuipika vyema pasipo kuikosea itakufanya utoe sauti nzuri.

Vyakula vyenye vitamin kama Vitamin A ikiwemo nyama ya ng’ombe lakini pia kutumia mayai,matunda mfano maembe,matikiti maji,mapeasi na  viazi vya njano.

Karanga pia ni moja ya chakula ambacho kinaweza kukufanya kama muimbaji uweze kuwa na sauti nzuri wakati wa kuimba.

Mbali na kutumia vyakula vyote hivi lakini pia muimbaji unapaswa kunywa maji ya moto kwa wingi na kufanya sauti yako kuendelea kuwa imara zaidi.
Lakini pia maji hayo unaweza kuchanganya pia na asali na ukanywa na kwa mchanganyo huo unaweza ukabadirisha sehemu kubwa ya sauti yako na kuwa ya mvuto kwa uimbaji wa aina yoyote.

Unywaji huu wa mchanganyiko wa asali na maji unaweza ukanywa siku moja kabla ya onyesho lako na kuweza kuitengeneza sauti yako kuwa yenye utofauti wa siku zote.

Vyakula ambavyo muimbaji hupaswi kuvitumia kabla ya kutumbuiza.

Tunajua kuwa kila chakula kina utamu wake pindi utumiapo lakini kunavyakula muimbaji hupaswi kuvitumia wakati unajiaandaa kutumbuiza mbele ya mashabiki wako kwakua vianaweza kusababisha kuharibu sauti yako.

Maziwa tunajua ni matamu kwa mnywaji lakini kwa muimbaji hupaswi kutumia kabla ya kuelekea kwenye kutumbuiza kutokana na kuwa yanaongeza Acid ambayo inaweza kukusababishia ukashindwa kutoa sauti iliyob ora zaidi.

Mbali na maziwa pia vyakula vyenye sukari unapaswa uviache kabla ya kuanza kutumbuiza mfano juisi iliyochanganywa na sukari kutokana na kuwa inatengeneza mabaki mabaki ndani ya kinywa chako yanayoweza kukusababishia ushindwe kutoa sauti kwa wakati na ikakusababishia sauti kukwama kwama.

Kitu kingine ni kahawa haupswi kuitumi kabla ya kufanya onyesho lako kutokana na kuwa sauti yako inapaswa kutoka kwa uzuri zaidi ili kuweza kuimba kwa ufasaha lakini utumiapo kahawa inatengeneza kubanwa kwa sauti yako.

Mbali na kahawa kitu kingine ambacho ni muimbaji hupaswi kuvitumia ni pamoja na soda,pilipili,chocolate,pombe ya aina yoyote na vitu kama hivyo.
Top of Form
Bottom of Form
Top of Form
Bottom of Form



Image result for xavi barcelona 
Mchezaji wa zamani wa Barcelona Xavi ameitahadharisha Real Madrid kuwa Malaga si timu rahisi na kuifunga kwenye uwanja wao wa nyumbani ni kazi ngumu.

Los Blancos sasa wanahitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano kuelekea mechi ya Jumapili ugenini dhidi ya Malaga wakati Barcelona wakivaana na Eibar.

Madrid wanapewa nafasi kubwa kuifunga Malaga lakini Xavi anaamini mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kiwango safi cha timu ya Michel ambayo imefungwa mechi moja tu katika nane za mwisho.

Wakati Xavi akiendelea kuiombea mema timu yake ya zamani anakiri kuwa itakuwa ni pigo kubwa kwa Madrid ikiwa hawatatwaa taji msimu huu.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget