Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

Wimbo wa “I Know Who I Am” wamtambulisha zaidi Sinach kimuziki



Image result for sinach

Na Nicolaus Kilowoko.


Osinach Kalu ni Mwanamuziki lakini pia ni mwandishi wa nyimbo za injili aliyezaliwa nchini Nigeria akiwa ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto saba wa mzee Kalu.

Osinach amezea kuuteka muziki wa njili duniani na kuwa moja kati ya wasii wanaopendwa zaidi na kumfanya awezae kubadirisha jina lake hilo na kutunia jina jingine.

Osinach amekuwa akifahamika kwa jina hilo lakini aliweza kubadirisha jina hilo la Osinachi na kuwa Sinach kutokana na yeye mwenyewe  kuona kuwa jina lake linashindikana kutamkwa nyema na kuona Sinach linaweza kuwa ni raisi kwa watu kuweza kulishika kirahisi na kuweza kulitamkika midomoni mwa mwao.

Mbali na muziki lakini pia Sinach alifanikiwa kufunga ndoa na mumewe Joseph Egbu mnamo mwezi June mwaka 2014 katika kanisa la Ikeja, mjini Lagos, nchini Nigeria.

Lakini pia Sinach mbali na kuwa muandishi wa nyimbo zake pia ni kiongozi wa dini katika kanisa mabalo yeye anasali na kuendelea kuongeza imani kwa watu kumuamini Mungu kwa kumsikiliza yeye kama kiongozi lakini pia kwa kusikiliza nyimbo zake.

Sinach mbali na kufanya muziki lakini aliwahi kukiri kukosa kuungwa mkono na baba yake ambaye hapendi mwanae afanye kazi hiyo ya muziki huku mwenyewe akiamini kuwa muziki ni ndoto yake na unaweza kubadirisha maisha ya watu kutokana na muziki.

Sinach ni mwanamuziki ambaye ameweza kuandika nyimbo takribani 200 huku pia akiweza kushinda tuzo mbalimbali kutokana na ubora wa kazi yake ya muziki.

Pamoja na kuwa ni nyota duniani lakini pia hata katika kazi za kumuabudu Mungu na siku zote amekuwa akiandika nyimbo ambazo zinaweza kuishi kizazi hadi kizazi na kuleta mabadiriko katika jamii.

Mnamo mwaka 2008 aliweza kushinda tuzo ya nyimbo bora ya mwaka katika wimbo wake wa “This Is Your Season” mbali na kushinda tuzo hiyo lakini nyimbo zake zimekuwa zikiibwa katika makanisa mbalimbali ulimwenguni na kuzidi kumfanya afahamike zaidi.

Mbali na kushinda tuzo hizo lakini pia Sinach ameweza kushinda tuzo za mwimbaji ambaye anaweza kusifu na kuabudi wakati akiwa jukwaani ukiwemo mwaka 2007, 2008 na 2009.

Na kati ya wimbo ambao unapendwa ulimwenguni kote kwa watoto na watu wazima ni ule wa “I Know Who I Am” alioutoa mwaka 2012 ambao mpaka kesho bado hauchuji wala hauchoshi masikioni mwa mashabiki wake kutokana na kugusa maisha yayao kwa asilimia kubwa.

Wimbo huu umekuwa ukitumika sana katika matukio mbalimbali ya kumsifu na kumuabudu Mungu lakini pia umekuwa wimbo wa wenye shida mbalimbali kuweza kujifariji wapatapo mataizo.

Umekuwa wimbo ambao wanachi wa Uganda na Kenya wamezidi kuupenda kutokana na matatizo mbalimbali ambayo walishawahi kukutana nayo hapo nyuma n ahata kumfanya yeye mwenyewe Sinach kufurahia kuona wimbo huu unambeba zaaidi kati ya nyimbo zake zote.

Lakini mbali na kuweza kutumbuiza nchini Nigeria Sinach ameweza kutumbuiza takribani nchi saba sasa ikiwemo nchi ya Kenya, katika kanisa la Citam Karen, Afrika kusini, Marekani, Trinidad, Tobago, na nchini Uganda katika kanisa la Miracle Centre Cathedral.

Sinach amekuwa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Nigeria na kumfanya kuwa mwanamuziki bora wakati wote kutokana na ubora wa nyimbo zake.

Ni mwanamuziki ambaye amekuwa na ndoto ya kubadirisha mawazo ya watu tangu alipokuwa mdogo na ndio kitu ambacho anakifanya kwa sasa kupitia nyimbo zake zenye ujumbe mzito wa kusisimua na zenye kufanya zinawabadirisha watu kimtazamo.

Mbali na kufanya kazi ya kuimba lakini Sinach amekuwa si mfanyabiashara katika nyimbo zake bali amekuwa mtu ambaye anawaza kuusogeza muziki wa injili mbali na kufanya uwe ndio maisha ya watu.

Kitu ambacho kwa miaka ya hivi karibu imekuwa ikiaminika kuwa muziki wa injili umekosa mvuto wake kutokana kuingiliwa na wakati mwingine ukifananisha kama muziki wa dunia.

Umekuwa ukifananishwa kama muziki wa duniani baada ya waimbaji wengi kufata mambo ya kidunia na kuyaingiza katika muziki huo na kuufanya ukose radha ya kuwa muziki wa injili.

Jambo hilo ndilo linalomfanya Sinach kwa upande wake kutotaka muziki wake kuwa kama biashara bali kuwa muziki ambao unaweza ukawaokoa watu wengi na kubadirisha mitazamo yao ya maisha.

Amekuwa akiimba nyimbo zake kutoka moyoni na kutoa nyimbo kutokana na maisha ya watu katika jamii husika na kutokata tamaa kwa yale mambo magumu aliyowahi kuyapitia.

Amekuwa akisistiza kila mara anapoulizwa juu ya wanamuziki ambao wamekuwa wakiimba muziki wa injili lakini ambao haunafaida katika jamii hukua akisisitiza kuwa Mungu ndiyo kitu cha kwanza alafu mwanamuziki ndiye anayefata.

Sinach amekuwa akitoa ushauri kila wakati kwa wanamuziki wenzake kutokana na mafanikio yake akielezea kuwa muziki wake unakuwa kwa kufanya maombi kwa Mungu hivyo wasitegemee wafadhiri katika kuwanyanyua kimuziki.





Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget