Kamati ya Taifa Stars imeanza kufanya kazi yake baada ya hii leo kutoa rasmi namba ambayo itakuwa ikitumika katika masuala ya kuisaidia na kuichangia timu ya Taifa ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Akiongea na waandishi wa habari, katibu wa kamati hiyoTeddy Mapunda amesema
watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia
shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668
(Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji,
uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa
utaratibu kwa ajili ya mashabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria
katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze
kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 1.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na
wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba
zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo
wa tarehe 14 Novemba, 2015
Post a Comment