Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma
salamu za rambirambi kwa Kocha Mkuu wa klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu
ya Meja Mstaafu Abdul Mingange kufuatia kifo cha mke wake Fatma Juma
kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake kwenda kwa familia ya marehemu,
TFF imempa pole mme wa marehemu Meja Mingange, ndugu jamaa, marafiki pamoja na
klabu ya Mbeya City kufuatia kifo hicho.
Mazishi ya marehemu Fatma Juma yamefanyika Jumapili
iliyopita katika makaburi ya Matombo mkoani Morogoro.
Post a Comment