Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema matumaini
yake ni kwamba kiungo wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa ametumwa
Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji.
Wilshere, mwenye miaka 24, ambaye huchezea timu ya
taifa ya Uingereza, alienda Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.
Ni mmoja wa wachezaji waliokua kutoka chuo cha
kustawisha wachezaji cha Arsenal na aliwachezea mechi yake ya kwanza 2008 akiwa
na miaka 16.
Lakini alicheza mechi tatu pekee klabu hiyo msimu
uliopita kutokana na majeraha na Wenger amesema walizungumza na mchezaji huyo
kihusu mustakabari wake.
Bournemouth watakutana na West Bromwich Albion
Jumamosi hii na Wilshere anatarajiwa kucheza.
Post a Comment