KIKOSI cha Simba kimeanza safari leo hii kuelekea
mjini Mtwara kwa ajili ya mechi yake ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili
keshokutwa Jumapili.
Mechi hiyo ya kwanza ya Simba itakuwa dhidi ya
Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kwa Simba, kitakuwa kipimo namba moja na
wanalazimika kushinda ili kuanza sahihi kwa kuwa tofauti yao na Yanga ni pointi
mbili tu.
Uwanja wa Nangwanda umekuwa ni mgumu kwa timu nyingi
kubwa za Ligi Kuu Bara na Simba lazima wawe makini.
Post a Comment