Homa ya pambano la Ligi Kuu
Tanzania Bara kati ya Azam na Yanga imeanza kupanda ambapo Azam FC wamesema
hawana mpango wowote wa kuiwekea kambi timu hiyo.
Mtanange huo wa kusisimua
utapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili hii.
Akizungumzia Mtendaji mkuu wa Azam
FC SAAD KAWEMBA amesema Yanga kwao ni timu ya kawaida sana hivyo hawaoni haja
ya kuweka kambi nje ya Chamazi.
Post a Comment