Klabu ya Liverpool inakaribia kumteua meneja wa
Borussia Dortmund Jurgen Klopp kuwa meneja wao mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka
mitatu.
Liverpool wanamatumaini ya kukamilisha majadiliano hayo siku ya
kesho na kumtaja meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 raia wa Ujerumani kuchukua
nafasi ya Brendan Rodgers mwishoni mwa wiki.
Rodgers alitimuliwa Jumapili kufuatia sare ya bao 1-1
waliyopata katika Ligi Kuu dhidi ya Everton.
Klopp ametakiwa kuwachukua
wasaidizi wake wa zamani Zeljko Buvaz na Peter Krawietz kuwa sehemu ya benchi
lake la ufundi.
Post a Comment