Winga Lukas Podolski ameondolewa katika kikosi cha
timu ya taifa ya Ujerumani ambacho kinajiandaa na mechi za kufuzu michuano ya
Euro 2016 dhidi ya Ireland na Georgia baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha
mguu.
Podolski alijiunga na kikosi hicho Jumatatu lakini
vipimo zaidi vilionyesha kuwa winga huyo wa Galatasaray hataweza kucheza katika siku
zijazo.
Katika mchezo wa kesho dhidi ya Ireland utakaochezwa
Dublin Ujerumani wanaweza kujihakikishia nafasi ya kufuzu michuano hiyo
itakayofanyika nchini Ufaransa mwakani.
Ujerumani ndio
wanaoongoza kundi D wakifuatiwa na Poland katika nafasi pili huku wakipishana
alama mbili.
Post a Comment