
Katika salam zake, Malinzi
amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja
na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi
alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali
zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya
Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira
wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja
katika kipindi hichi cha maombelezo.
Post a Comment