
Kocha Rafa
Benitez wa Real Madrid, amesema kuwa kikosi chake ni bora na ana uhakika
kitabeba ubingwa wa Hispania msimu huu.
Benitez
amesema Kumekuwa na taarifa nyingi ambazo si sahihi, za kuwa wachezaji wake
hawana amani klabuni hapo na kueleza kuwa wachezaji wake wana furaha na wako
tayari kwa ajili ya kubeba kombe au makombe.
Amesema
anaamini ana kikosi bora na wachezaji wanapenda na anaamini watafanya kitu bora
zaidi katika la liga msimu huu.
“Majeraha ya
mara kwa mara yanatuandama lakini tunaamini yatapita nasi tutaweza kupambana,”
alisema Benitezi.
Post a Comment