Kuelekea katika mtanage wa
kusisimua kati ya Yanga dhidi ya Azam fc TFF
imeeandaa mechi maalum ya viongozi wa dini ya Kiislamu watakocheza na
viongozi wa dini ya kikisto katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa
na na lengo la kudumisha amani kuelekea katika kipindi cha uchaguzi wa viongozi
wa kitanzania.
Akizungumza na kutoka
viwanjani Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam ALHAD MUSSA SALUM amesema mandalizi
kwa upande wao yamekamilika kuelekea katika mtanange huo na kuwataka watanzania
kufika uwanjani kushuhudia mtanange huo.
Naye OMARY MWAULANGA ambaye
ni balozi wa amani Tanzania
amesema ni vyema kuwa na michezo kama hiyo
baina ya viongozi hao wa dinina kuwataka vijana mbalimbali kwenda kushuhudia
mtanange huo ili kujifunza kuendelea kuimarisha amani ya kitanzania.
Post a Comment