
Timu ya Azam FC inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa kukuza soka la vijana unaojulikana kama ‘Azam FC Satelite Centre’ ili kuboresha soka la kitanzania.
Mradi huo utasimamiwa
na Kocha Mkuu mpya wa Academy ya Azam FC, Tom Legg raia wa Uingereza, ambaye
hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Azam FC, Saad Kawemba, amesema lengo kubwa la mradi huo ni kuzalisha wachezaji
bora vijana watakaopata nafasi ya kuingia kwenye academy (Azam FC) na wengine
kusajiliwa na timu nyingine.
Kawemba amesema kwa
kuanzia tu mradi huo utaanza na vituo vitano vitakavyokuwa kwenye mikoa mitano
tofauti nchini, kwenye kila mkoa zitaundwa timu nne za vijana za chini ya miaka
10,12,14 na16, huku akiongeza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 wanataka wawe
wamesambaza vituo hivyo nchi nzima.
Post a Comment