
Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imeanza kujifua huko
manungu turiani kwaajili ya mzunguko mwingine wa ligi kuu soka Tanzania bara
kwa mwaka 2015.
Afisa habari wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru amesema
timu yake hivi sasa imeingia katika ushindani zaidi baada ya kufanya vizuri
mpaka hivi sasa katika ligi kuu na kuleta upinzani kwa vilabiu vingine.
Kifaru amesema wameanza mapema mazoezi hayo ili
kujiweka vyema ili kuendeleza ushindani huo baada ya kuanza kwa mzugunguko
mwingine wa ligi.
Post a Comment