Ili kufanya timu kuwa bora zaidi kwa muda wote Uongozi
wa klabu ya soka ya African Sports inatarajia kufanya kikao na wanachama wake
kwajili ya kujadili maendeleo ya klabu hiyo baada ya kutofanya vizuri katika
ligi kuu soka Tanzania bara.
Khatibu Mwashamu ni afisa habari wa African Sports
amesema wanatarajia kufanya kikao hicho mapema mwezi huu baada ya kunza vibaya
kwa timu yako na kujadili jinsi gani ya kuiweka sawa.
Amesema ili klabu ifanye vyem ni lazima kuwe na
maboresho ya mara kwa mara na hicho ndicho wanachokitaka kukifanya kurejesha
imani kwa mashabiki wao.
Post a Comment