
Klabu ya soka ya Simba hatimae hii leo imeachana
rasmi na wachezaji wake Pape N’daw raia wa Senegal na Saimon Sserunkuma raia wa
Uganda ndani ya klabu hiyo baada ya kujiridhisha na mwenendo mbovu wa wachezaji
hao.
Akizungumzia kuachwa kwa wachezaji hao Afisa habari
wa msimbazi Simba HAJI MANARA amesema uongozi umeridhia na kuamua kuachana na
wachezaji hao baada ya kupokea ripoti ya kocha Mkuu wa klabu hiyo DYRAN KERR kutowahitaji
ndani ya kikosi chake kwa hivi sasa.
MANARA amesema pamoja na kuachana na wachezaji hao
klabu yao inamipango ya kuongeza wachezaji wengine ndani ya klabu hiyo katika
kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili hasa kumuongeza aliyekuwa mchezaji wao
PAUL KIONGERA na wachezaji wengine.
Kwa upande mwingine MANARA amefunguka kuhusu mipango
na maendeleo ya uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju huku akiwapuuzi wale wanaoibeza
klabu hiyo kuhusu maendeleo ya uwanja wa klabu hiyo kushindwa kuujenga kwaajili
ya matumizi ya wachezaji wake.
Aidha klabu ya soka ya simba inaendelea na mazoezi
yake kwaajili ya mzunguko mwingine wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Post a Comment