
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez amebainisha
kuelekea mchezo wao wa Clasico kuwa safu ya ulinzi ya Real Madrid ni ngumu
kuwahi kupambana nayo katika maisha yake ya soka.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay, aliichezea
Barcelona mechi yake ya kwanza dhidi ya Madrid katika Uwanja wa Santiago
Bernabeu Octoba mwaka jana.
Katika mchezo huo Barcelona ilitandikwa mabao 3-1 huku
Suarez akitoa pasi ya bao pekee lililofungwa na Neymar lakini walifanikiwa
kulipa kisasi katika mchezo wa maruadiano kwa yota huyo kufunga bao katika ushindi
wa mabao 2-1 waliopata.
Post a Comment