Nahodha wa timu ya taifa ya
Uholanzi, Arjen Robben amesema mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya
Wales ni nafasi ya kuanza kujijenga upya baada ya kushindwa kufuzu michuano ya
Euro mwakani 2016.
Akihojiwa Robben amesema jambo pekee
wanaloweza kufanya ni kujaribu na kuwanza kujijenga upya tayari kwa maandalizi
ya mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.
Uholanzi walishindwa kufuzu michuano
hiyo kwa kumaliza katika nafasi ya nne katika kundi lao pamoja na kupangwa kama
timu ya juu.
Robben mwenye umri wa miaka 31, toka
wakati huo amechukua beji ya unahodha kutoka kwa Robin van Persie na anataka
kuanza kwa kuifunga Wales ambao wamefuzu michuano hiyo.
Post a Comment