
Shirikisho la soka chini Tanzania TFF linaendelea
kuweka mikakati kwaajili ya timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars kwaajili ya
kuiimarisha zaidi katika mashindano mbalimbali yanayokuja mbeleni.
Akizungumza na Kilowoko.blogspot.com Mratibu wa timu za
Taifa MARTIN CHACHA amesema wanajipanga wao kama Shirikisho kuhakikisha timu
hiyo sasa inafanya jitihada zaidi ya kubaki katika kiwango kizuri cha soka.
Hii ni baada ya timu ya Twiga stars kuitandika timu
ya wanawake ya Malawi kwa mabao 2-0 jumamaosi iliyopita ukiwa ni mchezo wao wa
kirafiki katika uwanja wa Azam Complex.
Post a Comment