
Na Nicolaus Kilowoko.
Hatimaye Timu ya Taifa ya Tanzania
kwa upande wa soka la wanawake, Twiga Stars imekata mzizi wa fitna baada ya
hii leo kuitandika timu ya wanawake ya Malawi kwa mabao 2-0 katika dimba la Uwanja
wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam mchezo ambao ni wa kirafiki wa
kimataifa.
Mchezo huu wa Twiga Stars ulikuwa ni
sehemu moja wapo ya kumuaga mchezaji mwenzao ambaye aliyekuwa mwanzilishi wa
timu hiyo kwa kipindi kirefu mkongwe, Esther Chaburuma ‘Lunyamila’.
Katika mchezo huu Twiga ilikuwa na
moto wa aina yake kutokana na mchezo waliokuwa wanacheza kutokana na kasi ya
mchezo huo na kuwamili wenzao wa Malawi.
Twiga Stars ilipata ushindi huo
mnono wa mabao 2-0 kupitia kwa wachezaji wake mahiri na hatari kabisa Asha
Rashid katika dk.43 lingine likiwekwa kimiani na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ katika
dk.82 ya mchezo.
Ikumbukwe tu katika mchezo huo
kiingilio kilikuwa ni shilingi 1000 huku kikosi cha Twiga Stars kikiwa kinanolewa
na kocha mzawa Rogasian Kaijage huku akiwataka watanzania wajitokeze kwa wingi katika kuisapoti
timu hiyo kwa kuipatia udhamini wa kutosha.
Post a Comment