
Jijini Mbeya wenyeji Mbeya Warriors watakuwa wenyeji
wa Wenda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Sokoine jijini humo, huku katika
uwanja wa Majimaji mjini Songera timu ya Mighty Elephant watakua wenyeji wa
African Wanderes.
Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Changanyikeni FC
katika uwanja wa Ilulu, huku timu ya Sabasaba ya mjini Morogoro wakiwakaribisha
jirani zao Mkamba Rangers katika uwanja wa Jamhuri.
Michuano hiyo itaendelea kesho Jumatano kwa michezo
miwili, Polisi Morogoro watawakaribisha Green Warriors uwanja wa Jamhuri mjini
humo, huku timu ya Mshikamano FC wakiwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam.
Katika michezo iliyochezwa jana, Abajalo ilibuka na
ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Transit Camp, huku Pamba FC ya jijini Mwanza
ikiibuka na ushindi wa bao 1- 10 dhidi ya Bulyankulu FC ya mkoani Shinyanga.
Post a Comment