
Kocha wa washika mitutu wa Jiji La London
klabu ya Arsenal,Arsene Wenger amemsifia Mesut Ozil kuwa ni mchezaji bora wa Ligi Kuu
na kumfananisha na nguli wa klabu hiyo Dennis Bergkamp.
Sifa hizo zimekuja kwa Ozili kufuatia kiwango
kikubwa alichoonyesha katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya
Bournemouth usiku wa kuamkia leo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, alitengeza
bao moja na kufunga lingine katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa
Emirates na kufanya timu hiyo kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mpaka sasa Ozil ameshatoa pasi za mwisho 16 na
kufunga mabao matano katika ligi na kumfanya kukaribia rekodi ya pasi za mwisho
20 ambayo iliwekwa na nguli mwingine wa Arsenal Thierry Henry.
Akihojiwa
Wenger amesema ukitizama kiwango na idadi ya pasi za mwisho alizotoa msimu huu
hakuna shaka kuwa ndio mchezaji bora kwasasa nchini Uingereza.
Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kiungo huyo
kwasasa anakaribia kufanana na Bergkamp kwani pamoja na kutoa pasi lakini pia
amekuwa akifunga mabao muhimu.
Post a Comment