Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

TFF YAZUIA WACHEZAJI HAWA BAADA YA KUPITIA MAPINGAMIZI YAO.



 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Richard Sinamtwa, jana Jumatano ilikaa na kupitia malalamiko/pingamizi za usajili wa wachezaji yaliyokuwa yamewasilishwa TFF mara tu baada ya usajili wa dirisha dogo uliofungwa Disemba 15, mwaka huu.


Kamati hiyo imeweza kupitia na kupitisha usajili kwa vilabu mbalimbali, huku pia kamati hiyo ikizuia baadhi ya usajili wa wachezaji waliosajiliwa, mpaka pande hizo mbili zitakapomalizana ndipo mchezaji husika ataweza kuitumikia klabu yake mpya.

USAJILI UFUATAO UMEZUILIWA KWA MAELEZO YAFUATAYYO

1. AFRICAN SPORTS
i. Karim Hamud Juma aliyeombea kusajiliwa na African Sports akitokea PolisiTabora usajili wake
ii. Michael Victor Mgimwa kamati imezuia usajili wake mpaka hati ya uhamisho wa kimataifa umezuiwa mpaka timu mbili zitakapofikia makubaliano itakapotumwa toka Thailand, mchezaji huyu alikuwa anaitumikia Rio United ya Thailand.

2. MAJIMAJI SPORTS CLUB
i. Danny David Mrwanda na Lulanga Andrew Mapunda-kamati imezuia usajili wake mpaka vilabu viwili vya Majimaji inayotaka kumsajili na Lipuli iliyokuwa inawamiliki wachezaji hao zitakapokubaliana na kutuma kwa maandishi makubaliano yao TFF.

 3. MBEYA CITY
i. Kamati baada ya uchunguzi imejiridhisha kwamba mchezaji Tumba Sued aliyewekewa pingamizi na Coastal Union alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Coastal Union siku ya tarehe 12 June, 2014 na mkataba huu ulienda kushuhudiwa kwa mwanasheria siku ya tarehe 23 Agosti 2014, kushuhudiwa huku hakukubatilisha mkataba uliosainiwa tarehe 12 June 2014.

Hivyo kamati inamtangaza Tumba Sued kuwa mchezaji huru toka tarehe 11 Desemba na kwa sasa ni mchezaji halali na amepitishwa kuichezea Mbeya City ya Mbeya.

ii. Kamati pia inatoa onyo kali kwa klabu ya Mbeya City na imeagiza kesi hii ipelekwe kwenye kamati ya nidhamu kwa kuongea na mchezaji Ditram Nchimbi ambaye ni mchezaji halali wa Majimaji ya Songea ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili na Majimaji  tarehe 20 Oktoba 2014 hivyo mkataba wake utaisha tarehe 19 Octoba 2016. Mbeya City wameongea na mchezaji mwenye mkataba uliozidi miezi 6 bila kuomba ridhaa ya klabu inayommiliki ambayo ni Majimaji.

4. JKT RUVU
JKT Ruvu iliomba kumsajili mchezaji Hassan Dilunga kutoka Stand United kwa kufata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuongea na klabu yake ya Stand United na kupata kibali cha kumsajili Dilunga kutoka kwa uongozi halali wa Stand United kupitia kwa mwenyekiti na katibu wa Stand United. 

Pamoja na ruhusa kutoka kwa Stand United bado kuna mtu anayeitwa mratibu wa Stand United aliiandikia barua TFF akipinga usajili wa mchezaji huyu.

Kamati imesikitishwa na kiendo cha mtu huyu ambaye hatambuliki na TFF na wala siyo mtu anayepaswa kuwasiliana na TFF kwa kuingilia maamuzi ya viongozi halali wa Stand United na imeamuru mtu huyo anayeitwa Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kwa kupora mawasiliano ya Stand United wakati viongozi halali wanaotambulika kikatiba wa Stand United wapo.

Kamati imeamua mratibu Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili kufuatia kutofata na kuheshimu uongozi halali wa klabu ya Stand United.
 
5. NDANDA SC-RAMADHANI KIPALAMOTO
Klabu ya Ndanda SC ilileta maombi ya kumsajili mchezaji Ramadhani Salim Kipalamoto amabye alikuwa anachezea Abajalo SC ya Dar es Salaam, maombi haya yamekataliwa kwa kuwa mchezaji husika alikuwa pia ameombewa kusajiliwa na Kagera Sugar na klabu yake ya Abajalo ikatoa ridhaa ya mchezaji huyu kwenda Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
 
6. NDANDA SC-IBRAHIM IS-HAAK
Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji  imeridhia ombi la mchezaji Ibrahim Is-haki aliyedai klabu yake ya Ndanda SC kuvunja mkataba wake kwa kutomlipa hela yake ya usajili kama walivyokubaliana.

Mchezaji huyu amevunja mkataba wake baada ya maombi yake TFF kukubaliwa na mwakilishi wa klabu yake ya Ndanda SC, Edmund Njowoke ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Ndanda SC, na kamati imeridhia maombi ya timu ya Geita SC ya kutaka kumsajili.

Mchezaji Ibrahim Is-haak amepitishwa kuichezea timu ya Geita Gold SC ya Geita.

7. MWADUI SC
Kamati imeridhia pingamizi la klabu ya KMC ya Kinondoni kumzuia mchezaji Emmanuel Memba aliyeombewa kusajiliwa na Mwadui Sc kwa kutofata utaratibu. Kamati inaiagiza klabu ya Mwadui kuongea na KMC wamiliki wa mchezaji ili wawaruhusu kumt

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget