
Mwingereza Andy Murray amemshinda raia wa Australia
Sam Groth na kufika raundi ya tatu ya mashindano ya tenisi ya Australian Open.
Mchezaji huyo aliyeorodheshwa nambari mbili katika
mashindano hayo, alimshinda Groth kwa 6-0 6-4 6-1 katika kipindi cha saa moja
na dakika 30.
Groth, 28, hakupewa nafasi ya kutawala na Murray,
ambaye anatokea Scotland.
Murray, 28, sasa ameingia katika 32 bora ambapo
atakutana na Mreno Joao Sousa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne.
Mwingereza mwingine Johanna Konta alimshinda Zheng
Saisai kutoka Uchina 6-2 6-3 na kufika raundi ya tatu ya mashindano hayo upande
wa wanawake.
Post a Comment