Klabu ya soka ya Simba SC imefanikiwa kuichapa timu ya
Bukinafaso ya mkoani Morogoro kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa katika
dimba la uwanja wa wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Katika mchezo huo wa leo Simba SC waliutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi na kama wangekuwa makini wangeshinda mabo mengi zaidi.
Katika dakika ya 77 ya mchezo Hamisi Kiiza Diegoakaiandikia
Simba SC bao la kwanza akimalizia vyema pasi ya Abdi Banda.
Dakika ya 90 Said Hamisi Ndemla aliiandikia Simba SC goli
la pili kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari na kuipa Simba goli la
pili.
Hamisi Kiiza alihitimisha karamu ya mabao kwa
kuifungia Simba SC baola tatu kwa mkwaju wa penati uliopigwa katika dakika ya 3
ya nyongeza na kupelekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0.
Post a Comment