
Siku moja baada ya Mbwana Samatta kurejea katika klabu ya TP
Mazembe badala ya kwenda Ulaya kujiunga na Genk ya Ubelgiji, meneja wa mchezaji
huyo Jamal Kisongo ametoa sababu tatu za maamuzi hayo.
Akizungumzia kuhusu hili Kisongo alisema baada ya Katumbi
kuonekana kushikilia msimamo wake wa kutomruhusu Samatta kwenda Genk, ndipo
akaamua kumshinikiza nyota huyo arudi kwenye klabu yake ili amalizie mkataba
wake na baada ya hapo aondoke akiwa kama mchezaji huru.
“Hiyo ni sababu ya kwanza ambayo tunaona kwa kufanya hivyo
Katumbi lazima atakataa kuona Samatta anaondoka klabuni hapo akiwa kama
mchezaji huru, jambo ambalo halitompa faida mmiliki huyo,”alisema Kisongo.
Kisongo alisema udhalilishaji kilichotokea hivi karibuni cha
gazeti moja la udaku kuandika kwamba Samatta alifumwa hotelini akiwa na
mwanamke, hivyo wameona ni vema kumpeleka Congo ili kuepusha madhara
yatakayotokana na kuharibiwa kwa saikolojia yake kufuatia habari hizo za
uzushi.
Kisongo alisema kitendo cha Samatta kuendelea kukaa nchini
kingezidi kutoa mwanya kwa magazeti ya udaku kumchafua na hivyo kuzima kabisa
ndoto zake za kusonga mbele.
Baada ya kushinda tuzo yake ya mwanasoka bora kwa wachezaji
wanaocheza ndani ya Bara hilo, Samatta ambaye ni mshambuliaji wa TP Mazembe ya
Congo DR na timu ya taifa, Taifa Stars alitarajiwa kusafiri kwenda Ulaya lakini
safari yake ilikwama kufuatia klabu hiyo ya Ubelgiji kushindwa kuafikiana dau
na mmiliki Moise Katumbi.
Genk walikuwa wanataka kumsajili Samatta kwa dau ambalo
mmiliki huyo wa TP Mazembe hakuridhika nalo kwa madai kwamba bei hiyo hailipi.
Post a Comment