Mzunguko wa tatu wa michuano wa
Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) unatarajiwa kuendelea wikiendi
hii mpaka katikati ya juma lijalo kwa michezo 13 kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini.
Kesho Jumamosi michezo mitatu
itachezwa, mjini Morogoro Burkinfaso FC watawakaribisha Simba SC katika uwanja
wa Jamhuri mjini humo, Pamba FC watawakaribisha Toto Africans uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya Mshikamno FC katika
uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara.
Jumapili michuano hiyo itaendelea
kwa michezo mitatu, jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Friends
Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji watakua wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja
wa Amani Njombe, huku Stand United wakicheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja
wa Kambarage mjini Shinyanga.
Michuano hiyo itaendelea Jumatatu,
Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
mjini Tabora, Panone FC dhidi ya Madini FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi na
Africa Lyon wakiwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumanne Mtibwa Sugar watawakaribisha
Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa
Wambi Mafinga, Africa Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga, na
Geita Gold watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini
Geita.
Singida United watacheza dhidi ya
Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa Namfua mjini Singida, na mchezo wa
mwisho utachezwa Februari Mosi katika ya Wenda FC dhidi ya Mbeya City uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Mpaka sasa timu ya JKT Mlale pekee
ndio imeshafuzu kwa mzunguko wa nne baada ya kuiondosha Majimaji kwa mabao 2-1,
katia mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Post a Comment