
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa klabu ya
Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania bara kufuatia kifo cha Mwenyekiti
wake Hassan Mlilo kilichotokea jana katika hospital ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake, Malinzi amewapa
pole familia ya marehemu Hassan Mlilo, ndugu, jamaa, marafiki na klabu ya
Tanzania Prisons, na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini
amesema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Mwili wa marehemu Hassan Mlilo
unatarajiwa kusafirishwa leo mchana kuelekea mkoani Mbeya, ambapo mazishi
yanatarajiwa kufanyika kesho katika mji wa Rujewa mkoani humo.
Post a Comment