JKT RUVU YAAPA KUMSHIKA SHARUBU MNYAMA SIMBA SIKU YA KESHO TAIFA.
Baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa maafande wenzao JKT Mgambo klabu ya soka ya JKT Ruvu imesema kesho lazima impigishe kwata mnyama Simba katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mchezo wao wa kesho Afisa mteule daraja la pili Costantini Masanja amesema pamoja na kipigo kizito walichokipata kutoka kwa maafande wenzao hao lakini Kocha wao Abdalah Kibadeni kuna vitu ameviona na ameshavibadirisha tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya mnyama Simba.
Masanja amesema kufunwa ni jamabo la kawaida katika mchezo wa kandanda lakini amewataka mashabiki wa JKT Ruvu kutovunjika moyo na timu yao baada ya kupoteza katika mchezo wao uliopita na sasa wanachotakiwa ni kuunganaa kwapaoja na kuiunga mkono timu hiyo katika kipindi hiki.
Post a Comment