Baada ya klabu ya soka ya Simba kutaka kumchukua kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kocha Hemed Morocco kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema lenyewe haliwezi kuingilia uhuru wa kocha huyo juu ya suala hilo.
Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema wao kama shirikisho hawawezi kuingilia uhuru wa kocha huyo ilimradi yeye mwenyewe akikubaliana na kuifundisha klabu hiyo.
Kocha Morocco anawaniwa na klabu ya Simba kuchukua mikoba iliyoachwa na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Dlyan Kerry baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtimua kwa kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo.
Morocco anawaniwa na Simba kusaidiana na kocha mwenzake Jackson Mayanja aliyetua klabuni hapo mapema wmezi huu kuwa kama kocha msasidizi kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha msaidizi Suleimani Matola.
Post a Comment