Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

RAIS SHEIKH SALMAN ATEMBELEA WIZARA YA HABARI.



 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa leo ametembelea Wizara ya habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.


Rais huyo leo alitembelea Wizara hiyo huku akiwa na mwenyeji wake katibu wa Wizara ya habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabrieli.


Katika mazugmzo hayo, Sheikh Salman ameielezea Serikali ya Tanzania nia ya FIFA kuendelea  kushirikiana na Serikali na TFF katika kuendeleza programu mbalibali za maendeleo ya mpira hasa wa vijana na wanawake.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Elisante  ameihakikishia FIFA kuwa nia ya Serikali ni kuona mpira unakua nchini na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TFF na FIFA ili kufikia azama hiyo.

Aidha pia ametoa wito kwa AFC kusaidiana na TFF katika masuala ya exchange programmes ili vijana wetu wapate uzoefu wa nje.

Sheikh Salman na ujumbe wake walitembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wakiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na shirikisho, ikiwemo uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.


Lakini Rais Sheikh Salman alipowasili jana alipokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili. 
 

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget