
Kamati ya kuratibu mashindano ya
urembo ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Juma Pinto imetangaza
kujitoa kwenye jukumu la kuratibu mashindano hayo baada ya kupishana katika
baadhi ya mambo ya kiutendaji ya kamati hiyo.
Kamati hiyo ikiwa na viongozi
wakiwemo Jokate Mwengelo, Juma Pinto na Gladys Shao imetangaza maamuzi hayo leo
wakati ikiongea na wanahabari jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Juma
Pinto amesema kuna mambo bado hayajatakaswa hasa kuhusiana na skendo ya
kughushi umri iliyoitafuna kamati iliyopita, hivyo wanahofu kwamba doa hilo
litaendelea kuwachafua.
Mwaka juzi mashindano hayo
yalikumbwa na skendo ya kughushi umri kwa aliyekuwa Miss Tanzania kwa wakati
huo Sitti Mtemvu, jambo lililomfanya avue taji na kumpa Lilian Kamazima.
Kama hiyo haitoshi Serikali kupitia
Baraza la Sanaa la Taifa BASATA iliyafungia mashindano hayo kwa kipindi cha
miaka miwili.
Skendo hiyo iliilazimu kamati
iliyopita chini ya Hashim Lundenga kujivua gamba na kuwakabidhi jukumu Juma
Pinto na jopo lake.
Post a Comment