Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na klabu ya soka ya Yanga Peter Manyika ameendelea na program yake ya mafunzo maalumu kwa nafasi ya ulinda mlango katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa walinda milango chipukizi.

Manyika amesema kwa sasa wanachoangalia ni kuangalia
jinsi gani ya kupata angalau nafasi kwa nchi za nje kwaajili ya kupeleka
chipukizi hao ambao wanaonekana kufanya vizuri zaidi.
Manyika amesema changamoto kubwa anayokutana nayo ni
idadi ndogo ya makipa chipukizi wanawake ambao kwa upande wa kwenye kituo chake
wameone kana kuwa wachache ukilinganisha na idadi ya makipa wanaume
Post a Comment