Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

KERR ASEMABADO YUPO YUPO SANA JIJINI DAR ES SALAAM HADI SIMBA WAMLIPE MPUNGA WAKE.


 
Baada ya Uongozi wa klabu ya soka ya Simba kumtimua kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba, Dylan Kerr hatimaye ameibuka na kumesema bado yupo yupo sana jijini Dar es salaam akisubiri malipo yake ikiwemo mshahara wa miezi miwili iliyopita ambao hajalipwa na uongozi wa klabu hiyo.

Kerr amesema bado anaidai klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi K/koo na asingependa kulizungumzia hilo kwa upana kutoka bado anaendelea kusubiri malipo yake kotoka katika uongozi wa klabu hiyo.

“Sitaki kuzungumzia sana suala la kufukuzwa kwangu lakini kwa kifupi bado nipo nasubiri viongozi wangu waniite ili tumalize suala hili bado nafuatilia malipo yangu sijalipwa miezi miwili kwa hiyo naomba tusiliongelee sana," Alisema Kerr.

Kerr ianaonyesha wazi kuwa alikuwa akifanya kazi katika klabu hiyo kigumu kwa kipindi cha miezi miwili sasa hajalipwa na huwenda iliwa ni moja ya klabu hiyo kufaya vibaya katika kombe la Mapinduzi kule visiwana Zanzibar.

Kerr ambaye ni raia wa nchini Uingereza ameiongoza Simba katika mechi 13 za Ligi Kuu soka Tanzania bara na kushinda michezo 8 ktoka sare michezo 3 kna kapoteza michezo 2 katika ligi hiyo.

Kwa upande wa mechi za jumla tangu atue nchini kuinoa timu hiyo, Kerr ameiongoza Simba katika jumla ya mechi 30 ambapo 19 kati ya hizo alishindsa na kufungwa mechi 5 huku 6 ikiwa ni sare.

lakini kwa Tathimini hii bado kocha huyo alikuwa anauwezo wa kufanya mambo makubwa katika klabu hiyo na kuipeleka mbali zaidi katika mashindano tofautitofauti.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget