
Klabu ya soka ya JKT Ruvu imefanya mazoezi yake hii
leo kwaajili ya kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo JKT mchezo utakaopigwa katika
viunga vya uwanja wa karume jijini Dar es Salaaam.
Ligi kuu Soka inatarajiwa kutimua vumbi lake tena
January 16 mwaka huu katika viwanja kadhaa baada ya kupumzika kwa muda kupisha
kombe la mapinduzi lililofanyika visiwani Zanzibar.
Kocha mkuu wa klabu ya JKT Ruvu Abdalah King
Kibadeni Mputa amesema lengo la mazoezi yao ya leo ni kujiweka sawa kwaajili ya
mchezo wao huu huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kujituma vizuri wanapokuwa
mazoezini.
Kwa upande wake Nahodha wa klabu hiyo George Minja
amesema hawana wasi wasi juu ya mchezo wao huo kutokana na mazoezi wanyoendelea
kuyafanya huku wakipata mbinu nyingi za kuwakabili wapinzani wao kutoka kwa
kocha wao.
Post a Comment