
Kamati ya mashindano ya Ligi ya mkoa wa Dar es
Salaam imeshusha rungu la adhabu kwa klabu ya FC Panama inayoshiriki ligi hiyo
baada ya kufanya fujo katika mchezo wao dhidi ya Makumba FC na kumshambulia
vikali mwamuzi wa mchezo huo.
Fujo hizo zilitokea baada ya Mchezo huo wa ligi ya
mkoa wa Dar es Salaam ulichezwa katika uwanja wa kunduchi kumalizika na
wachezaji hao walimvamia mwamuzi huyo na kumchezeshea kipigo kilichosababisha
mwamuzi huyo kupata majera ya mwilili.
Katibu wa Mashindano hayo Daud kanuti amesema klabu
hiyo sio mara yao ya kwanza kufanya tukio kama hilo kutoka na kuwa walishafanya
tukio kama hilo katika misimu ya ligi hiyo iliyopita.
Post a Comment