
Kiungo wa klabu ya soka ya Swansea City, Jonjo
Shelvey, Leo amefanyiwa vipimo vya afya katika makao makuu ya klabu ya soka ya Newcastle United ili kukamilisha Uhamisho wake wenye thamani ya Pauni Milioni 12.
Shelvey anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na kocha
mkuu wa wa klabu hiyo Steve McClaren baada ya kumsaini Henri Saivet kutoka
Bordeaux kwa Mkataba wa Miaka Mitano na Nusu.
Shelvey, mwenye Miaka 23, alisainiwa na Swansea Julai
2013 kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 5 na kuichezea Swansea Mechi 77 na
kufunga Bao 9.
Post a Comment