
Klabu ya soka Arsenal imethibitisha kusaini kiungo
wa klabu ya FC Basel Mohamed Elneny baada ya kusikika kwa minong’ono mingi ya
kumtwaa mchezaji huyo.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba
klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel ili kukiongezea kasi kikosi
chake katika harakati za kuwani ubingwa wa ligi kuu.
Kutokana na kusajiliwa kwa kiungo huyo sasa klabu ya
Arsenal inaweza ikamtumia katika mchezo wake wa jumapili watakokutana na klabu
ya anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.
Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu the Gunners £5m
kutua katika klabu hiyo yeye maskani yake jijini London.
Wenger amesema kiungo huyo amejiunga nao na
watajaribu kumchezesha katika mchezo wao wa jumapili kuona kama ataweza.
Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea
msimu wa 2013-14.
Post a Comment