
Vita ya kuwania kupanda daraja msimu ujao itaendelea
wikiendi hii kwa michezo 12 ya Ligi daraja la kwanza nchini (Startimes League)
kuchezwa katika viwanja mbalimbali kwa makundi A, B, C, kwa kila timu kusaka
pointi tatu muhimu.
Jumamosi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji
Polisi Dodoma watakua wenyeji wa Africa Lyon, Kiluvya United wakiwakaribisha
Mji Mkuu (CDA) katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Polisi Morogoro dhidi ya
Kimondo FC uwanja wa Jamhuri, huku Kurugenzi ikiwakaribisha Burkinafaso kwenye
uwanja wa Wambi mjini Mafinga.
JKT Mlale watawakaribisha Njombe Mji uwanja wa
Majimaji mjini Songea, Panone dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ushirikia Moshi,
Polisi Mara watakua wenyeji wa Rhino Rangers uwanja wa Karume mjini Musoma,
huku JKT Oljoro wakiwaribisha JKT Kanembwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
Ligi hiyo ya itaendelea siku ya Jumapili
kwa michezo minne kuchezwa, Friends Rangers watakua wenyeji wa Ashanti United
uwanja wa Karume, Polisi Dar dhidi ya KMC uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli
wakicheza dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Wambi Mafinga huku Polisi Tabora
wakicheza dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora.
Post a Comment