Klabu ya soka ya Liverpool usiku wa kuamkia hii leo
ilifanikiwa kuanza vyema michuano ya Capital One Cup baada ya kuitandika klabu
ya Stoke City bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo.

Liverpool walipata bao lao la shida kupitia kwa mchezaji wao Jordon Ibe katika dakika ya 37 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na kuleta ndoto mpya kwa klabu hiyo kufanya vizuri katika mechi zinazofata.
Kwa ushindi ambao wameupata Liverpool umeibua furaha
kwa kocha wao Jurgen Klopp na kumpa matumaini ya kutinga fainali ya michuano
hiyo.

Iwapo watafanikiwa mechi ya marudiano, Liverpool
watakutana na mshindi wa nusu fainali kati ya Everton au Manchester City,
kwenye fainali ambayo itachezewa uwanja wa Wembley.
Mechi ya kwanza ya nusu fainali hiyo nyingine
itapigwa usiku wa leo ambapo Everton watakuwa nyumbani Goodson Park dhidi ya
Manchester City.
Post a Comment