
Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na kati
imethibitisha kuwa nchi ya Sudan ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya
Kombe la Cecafa mwaka huu.
Nchi ya Sudani iliandaa michuano hiyo ya Cecafa kwa
mara ya mwisho mwaka 2013.
Nayo nchi ya Uganda imetangazwa kuwa itakuuwa
mwenyeji wa michuano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 yaani Cecafa
Under-17 na pia michuano ya ubingwa upande wa wanawake mwaka kwa huu.
Tukiachana na Sudan na Uganda nayo nchi ya Burundi
itakuwa mwenyeji wa fainali za wachezaji wa chini ya miaka 20.
Cecafa pia imeelezea mpango yao ya miaka mitano ambayoitasaidia
maendeleo ya soka kwa upande wa soka la vijana na wanawake pamoja na kuimarisha
uwezo wa kiufundi.
Lakini naya Rais wa Shirikisho la Soka la Somalia
Abdiqani Said Arab akiteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Cecafa.
Post a Comment