
Aliyekuwa kocha wa klabu ya Bayern Munich Pep
Guardiola ameelezea sababu ya kutoongeza Mkataba wake wa kuifundisha klabu hiyo ya Bayern
Munich kuwa anataka kuwa Maneja katika Ligi ya nchini Uingereza.
Kocha huyo mwenye miaka 44 bado hajajua atafundisha
timu gani baada ya kuondoka nchini Ujerumani ila amesema anataka kupata
changamoto mpya nje ya Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City inania ya kumuhitaji kocha
huyo Guardiola katika kipindi kijacho cha msimu wa ligi kuu soka nchini
Uingereza.
Lakini klabu ya Arsenal, Chelsea na Manchester
United nazo pia zinahusishwa na kuhitaji hudumu ya Guardiola, ambaye mkataba
wake unaisha mwaka huu na klabu yake ya Bayern na bado hajachagua klabu ya kujiunga
nayo.
Post a Comment