
Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Chelsea Guus Hiddink amesema
majeraha yanayomsumbu mchezaji wake Radamel Falcao’s ni makubwa sana na
anashindwa kuelezea ni lini hasa mchezaji huyo atarudi katika hali yake ya
kawaida.
Falcao ambaye ni raia wa nchini Colombia alikuwa
anajitahidi kurudisha kiwango chake Stamford Bridge katika kipindi hiki kwa
kuisaidia The Blues, lakini imeshindikana kutokana na kuwa na matatizo makubwa
yanayomsumbua.
Hiddink amesema mshambuliaji huyo anaweza akakaa nje
ya dimba kwa muda wa zaidi ya miezi miwili hadi kurudi katika hali yake ya
kawaida.
Wakati makubwa ya Falcao yakisumbu Hiddink tena
anailaumu klabu yake ya Chelsea baada ya
kumuuza mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kutokana na kuwa mchezaji huyo
ameonekana kuimarika zaidi katika timu yake.

Lukaku alishindwa kuonyesha manjonjo yake katika
kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho's na kuuzwa katika klabu ya Everton kwa dau
la £28 million mwaka 2014.
Mchezaji huyo mwenye miaka 22 ameonekana kucheza
vizuri katika ligi ya Uingereza huku Hiddink akiiombo klabu yake ya Chelsea's
kuwapa nafasi vijana wadogo kuonyesha vipaji vyao baada ya Lukakau hivi sasa
kuwasumbua hata walipokutana dhidi ya klabu yake ya Evarton.
Post a Comment