Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA TENA SIKUA YA KESHO.



 
Ligi Daraja la Daraja la Kwanza nchini natarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo kumi na mbili kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.


Kesho Jumamosi michezo tisa ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Katika uwanja wa Karume jijini Dar es salam mchezo kati ya Ashanti United dhidi ya Polisi Dodoma, Polisi Morogoro watawakaribisha Kurugenzi FC ya Mafinga katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Kimondo FC wakicheza dhidi ya Burkinafaso kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Maafande wa Ruvu Shooting watacheza dhidi ya Mji Njombe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli dhidi ya JKT Mlale katika uwanja wa Wambie mkoani Iringa, maafande wa JKT Kanembwa wakiwakaribisha Mbao FC katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Geita Gold watawakaribisha Polisi Mara kwenye uwanja wa shule ya Nyankumbu mjini Geita, JKT Oljoro watacheza dhidi ya Rhino Rangers uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, huku maafande wa Polisi Tabora wakiwakaribisha Panone FC katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Karume, huku timu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) wakicheza dhidi ya Friends Rangers katika uwanja wa Mlandizi Mabatini.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget