Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

CECH ASEMA MESSI AJIPANGE SANA KUMFUNGA YEYE.



 

Mlinda mlango wa Arsenal, Petr Cech amekiri kupania kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa na nyota wa Barcelona Lionel Messi.


Akihojiwa Cech amesema ni jambo kubwa kwa kuwa sio makipa wengi ambao wamewahi kucheza na Messi katika mechi nane na hajawafunga.

Wawili hao wamekutana mara kadhaa wakati Cech akiwa Chelsea ambapo katika mechi nane walizokutana Messi hajafanikiwa hata mara moja kumfunga golikipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech.

Nyota hao wanatarajiwa kukutana tena wakati Arsenal watakapovaana na Barcelona katika hatua ya timu 16 bora za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi ujao.


Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget